Hali Ya Afya Ya Trump Yachunguzwa Baada Ya Wikendi Iliojaa Hofu

 

Rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kupewa uangalizi wa karibu akiwa hospitali ambako anapokea matibabu ya Covid-19.

Kuna tashwishi kuhusu uwezekano wa Bw. Trump kutolewa hospitali - kama walivyokuwa wamesema madaktari wake kwamba huenda akatoka Jumatatu huku maswali yakiibuliwa kuhusu hali yake.

Kiwango cha oksijeni yake kilishuka mara mbili na pia anatiliwa tiba ya steroid. Siku ya Jumapili, aliushangaza umma alipoonekana hadharani akiendeshwa kwenye gari kuwasalimu wafuasi wake, hatua ambayo ilikosolewa vikali.

"Zaidi ya Wamarekani 205,000 wamefariki. Tunataka uongozo. Sio picha na video," aliandika

Kwenye Twitter yake Hakeem Jeffries, mwenyekiti wa Democrats katika bunge la Wawakilishi. Akiwa amevalia barakoa, rais alipunga mkono kutoka ndani ya gari muda mfupi baada ya kuandika ujumbe kwenye mtandao wake wa Twitter akisema kwamba atafanya "ziara ya kushutukiza".

Bw.Trump, ambaye amekosolewa kwa jinsi alivyoshughulikia janga la corona, pia alisema amejifunza mengi kuhusu virusi hivyo.

Awali, madaktari wake walisema Bw. Trump anaendelea kupata nafuu na kwamba huenda akatolewa hospitali kufikia Jumatatu.

Dk Sean Conley alisema kiwango cha hewa ya oksijeni cha rais kilishuka mara mbili tangu alipogunduliwa kuwa na virusi vya corona, na ameanza kutumia dawa inayofahamika kama dexamethasone.

Rais aliongezewa oksijeni ya ziada mara moja baada kuthibitishwa kuwa na virusi, alisema Dk Conley, ambaye pia alifafanua mkanganyiko uliosababishwa na taarifa tofauti kuhusu hali ya Bw. Trump.

Katika ujumbe wa Twitter, rais - aliyekuwa amevalia suti, koti na shati bila kufunga tai - alisema: "Nimejifunza mengi kuhusiana na Covid" Nimejifunza kwa kwenda shule haswa.

Hii ni shule halisi. Hii sio shule ya njoo tusome vitabu. Sasa naona na nimeelewa. Ni jambo la kuvutia sana, hivi karibuni nitawafahamisha."


EmoticonEmoticon