Hatua Za Ufaransa Kudhibiti Corona Kubakia Zaidi Ya Desemba 1

 

Hatua kali mpya za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona zilizotangazwa na Ufaransa zinaweza kuongezewa muda zaidi ya tarehe ya mwisho ya Desemba mosi, kulingana na Profesa Jean-Fran├žois Delfraissy mshauri wa serikali wa masuala ya kisayansi. 

Rais Emmanuel Macron amesema jana kwamba Ufaransa huenda ikaanza kupunguza vikwazo hivyo pale maambukizi ya virusi vya corona yatakapoanza kupungua na kufikia 5,000 kwa siku badala ya idadi ya hivi sasa ya maambukizi 40,000 kwa siku moja. 

Lakini Delfraissy amesema haamini kama hilo linaweza kufanikiwa ifikapo Desemba mosi. Viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana leo kwa mkutano wa njia ya video kujadili namna ya kuudhibiti mgogoro huo wa virusi vya corona, kulingana na vyanzo vya Ulaya.


EmoticonEmoticon