Ifahamu Ndege Mpya Ya Abiria Inayoweza Kusafiri Kwa Kasi Zaidi Ya Sauti

 

"Watu mara kwa mara wametaka kusafiri kwa haraka , tangu mtu wa kwanza kusafiri katika mabonde kwa kutumia farasi , anasema Mike Bannister.

Bwana Bannister alisafiri kwa kutumia ndege ya Concorde kupitia kampuni ya ndege ya British Airways kwa takirban miaka 22.

Kama rubani mkuu wa ndege hiyo aliendesha ndege hiyo juu ya anga ya London mwezi Oktoba 2003 huku safari yake ya mwisho ikiwa ile alipotua na ndege hiyo katika makavazi ya Bristol.

Karibia miongo miwili baadaye ulimwengu unakaribia kuwa na ndege ya abiria inayoweza kusafiri kwa kasi zaidi ya kasi ya sauti.

Mwezi Huu , kampuni ya ndege ya Boom Supersonic ilianza kufanyia majaribio ndege yake aina ya XB-1 Supersonic.

Ndio ndege ya kwanza aina ya Supersonic ya raia tangu ndege ya Urusi ya Tupolev TU -144 mwaka 1968. Ndege hiyo nyembamba itajaribiwa.

Inatarajiwa kubeba kati ya abiria 65 na 88 kupitia njia za anga ya bahari. Shirika la Nasa lina ndege za kushangaza zaidi zenye mabawa madogo.

Hii itapaa mnamo 2022, ikifuatilia tuzo ya ndege endelevu zaidi.

Pia kuna kamapuni ya kutengeneza ndege ya Aerion, inayosema kwamba aina yake ya ndege itatoa ndege yenye kasi zaidi kufikia mwisho wa muongo huu.

Lakini ikiwa na uwezo wa kubeba kati ya abiria 8 hadi 10 ndege hiyo ya AS2 inalenga soko tofauti ya baishara ya usafiri wa anga za juu .


EmoticonEmoticon