Iran imeonya
kuwa mapigano mapya kati ya majirani zake Azerbaijan na Armenia yanaweza
kuongezeka na kuwa vita pana ya ukanda.
Rais
Hassan Rouhani alisema ana matumaini "ya kurejesha utulivu" katika
eneo hilo kufuatia siku kadhaa za mapigano makali yanayosababishwa na eneo
lenye mgogoro la Nagorno-Karabakh.
eneo
hili ni sehemu rasmi ya Azerbaijan lakini inadhibitiwa na jamii ya Waarmenia.
Mapigano
ya sasa ni mabaya zaidi kuwahi kutokea katika miongo kadhaa, na pande zote
mbili zimelaumiana kwa machafuko .
"Lazima
tuwe waangalifu kwamba vita kati ya Armenia na Azerbaijan isiwe vita vya
kieneo," Rais Rouhani alisema Jumatano.
"Amani
ndio msingi wa kazi yetu na tunatarajia kurejesha utulivu katika eneo hili kwa
njia ya amani," ameongeza.
Rais
Rouhani pia alisema "haikubaliki kabisa" kwa makombora yoyote
yaliyokosea njia kutua kwenye ardhi ya Irani.
Maoni
yake yalifuatia ripoti kwamba makombora yalikuwa yametua kwenye vijiji vya
Irani, karibu tu na mpaka wake wa kaskazini na Armenia na Azerbaijan.
"Kipaumbele chetu ni usalama wa miji na vijiji vyetu," Rais Rouhani alisema.
EmoticonEmoticon