John Cena Afunga Ndoa Ya Siri Na Mpenzi Wake Mpya

 

Muigizaji na mwanamieleka maarufu John Cena amefunga ndoa na mpenzi wake Shay Shariatzadeh mjini Tampa Florida, imeripotiwa. Wawili hao walianza mahusiano mapema mwaka 2019 kufuatia Cena kuachana na aliyekua mchumba wake, Nikki Bella mwaka 2018.

Cena na Shay walivishana Pete ya uchumba kwa siri na pia walifunga ndoa ya siri Oktoba 12 mwaka huu mjini Florida. Shay alizaliwa nchini Iran lakini ni raia wa Canada.

Hii ni ndoa ya pili kwa John Cena, awali alimuoa Elizabeth Huberdeau mwaka 2009 na walitalikiana mwaka 2012.


EmoticonEmoticon