Juventus Wajitenga Sababu Ya Corona

 

Wachezaji wa Juventus wote wamelazimika kujitenga kwa ridhaa yao baada ya kiungo wa timu hiyo Weston McKennie kuthibitika kuwa na Corona.

Weston McKennie ambaye amejiunga na Juventus katika dirisha hili la usajili akitokea Schalke ya Ujerumani, ndio mchezaji pekee wa Juventus kuthibitika kuwa na maambukizi hayo kati ya wachezaji wote hivyo wanajitenga kwa tahadhari.

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni saa 24 zimepita toka Cristiano Ronaldo wa Juventus athibitike pia kuwa na maambukizi ya Corona akiwa kwao Ureno  na sasa amejitenga.


EmoticonEmoticon