Je unajua
kuwa Kanisa la England yaani Church of England ni wamiliki wenza wa wimbo wa
Beyoncé wa Single Ladies, wimbo wa Rihanna maarufu kama Umbrella, na ule wa
Justin Timberlake uliovuma SexyBack?
Unaweza ukastaajabisha lakini kanisa
hilo ni miongoni mwa wawekezaji 100 katika kampuni inayoitwa Hipgnosis, ambayo
kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita, wamepata haki ya maelfu ya nyimbo.
Hadi kufikia
sasa, kanisa hilo limetumia zaidi ya bilioni 1 kwa muziki ulioimbwa na Mark
Ronson, Chic, Barry Manilow, na Blondie.
Aidha, pia limefanikiwa kuingia kwenye umiliki wenza wa nyimbo kama vile za Boyz II Men inayofahamika kama End Of The Road, wa Whitney Houston unaojulikana kama I'm Your Baby Tonight, na ule wa Bobby Brown wa Don't Be Cruel.
EmoticonEmoticon