Kansela Merkel Aonya Kuhusu Ongezeko La Corona Ujerumani

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameonya kuwa nchi yake huenda ikapoteza udhibiti wa janga la virusi vya corona kama majimbo yenye idadi inayoongezeka ya maambukizo hayataimarisha hatua za kupambana na virusi hivyo. 

Kuafutia mkutano wa video na mameya wa miji 11 mikubwa ya Ujerumani, Merkel ameonya kuhusu kutokea kwa maambukizo mengi kama mamlaka za afya hazitaweza kumudu ufuatiliaji wa watu walioambukizwa. 

Kansela Merkel ameonya kuwa maeneo yanayoshuhudia idadi kubwa ya maambukizo yatapewa siku kumi kupambana na takwimu hizo zinazoongezeka kabla ya hatua kali kuchukuliwa. 

Taasisi ya afya ya umma nchini Ujerumani, ya Robert Koch imeripoti maambukizo mapya 4,516 katika kipindi cha siku moja, na kufikisha 314,660 jumla ya idadi ya maambukizo.


EmoticonEmoticon