Kauli Ya Arnold Schwarzenegger Baada Ya Kufanyiwa Upasuaji Wa Moyo

 

Muigizaji wa filamu na aliyekuwa Gavana wa jimbo la Califonia-Marekani, Arnold Schwarzenegger ameruhusiwa kutoka hospitali baada ya kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Gavana huyo ameruhusiwa Ijumaa hii na kuwashukuru wahudumu wa Cleveland Clinic kwa kumsadia kupata auheni."Ninajisikia mzuri na tayari nimekuwa nikitembea katika mitaa ya Cleveland nikifurahiya sanamu mbalimbali. Asante kwa kila dokta na muuguzi kwenye timu yangu," alitweet pamoja na picha zake akiwa kitandani kwake na akitembea kuzunguka jiji

Huu si upasuaji wa kwanza kwa muigizaji huyo, ambapo upasuji wa awali ulifanyika mwaka 2018. Mwaka 1997 Schwarzenegger alikuwa amewekewa mirija kwa sababu ya kuwa natatizo katika moyo wake wakati alipokuwa amezaliwa ilibidi abadirishwe.


EmoticonEmoticon