Derek Chauvin, Askari ambaye
alishtakiwa kwa kosa la kumuua Mmarekani mweusi George Floyd ataruhusiwa kuishi
nje ya eneo alilokuwa anaishi la Minnesota, USA wakati akisubiri hukumu yake
hii baada ya kuachiwa kwa dhamana yenye thamani ya USD Milioni moja, hukumu yake
inatarajiwa kutolewa Mwezi March mwakani kufuatia Mahakama kumkuta na hatia ya
mauaji
Hatua hii ya Derek
kuruhusiwa kwenda nje ya Minnesta inakuja ili kuokoa usalama wake kutokana na
Watu kuwa na hasira nae, Askari huyo alikuwa Gerezani tangu May 31 baada ya
video yake kusambaa akimkanyaga George Floyd shingoni hadi akakosa pumzi na
kufariki Dunia, tukio ambalo liliibua maandamano makubwa Marekani na Mataifa
mengine Duniani,
"Tayari baada
ya kutangazwa kuwa ameachiwa kwa dhamana Derek ameanza kupokea meseji za
vitisho na eneo analoishi limeonekana kuwa hatari kwake, atahamia kwingine
hususani maeneo ya Dakota Kusini, Dakota Kaskazini, Iowa au Wisconsin,
atazijuza Mamlaka ni wapi ataenda kuishi"-MAHAKAMA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon