Kiongozi wa
Kanisa katoliki duniani Papa Francis amesema kwamba anafikiria wapenzi wa
jinsia wanastahili kuruhusiwa "kuoana".
Wachambuzi
wanasema kauli yake hiyo imeashiria wazi msimamo wake kuhusu uhusiano wa
kimapenzi wa watu wa jinsia moja, katika makala yaliyoelekezwa na Evgeny
Afineevsky.
"Watu
wanaoshirika mapenzi ya jinsi amoja wana haki ya kuwa na familia,"alisema
katika filamu, ambayoilioneshwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumatano.
"Ni
watoto wa Mungu nawana haki ya kuwa na familia. Hakuna mtu anayestahili
kutengwa ama kufanywa ajihisi mnyonge kwa kuamua kuwa katika uhusiano wa aina
hiyo.
"Tunachopaswa
kuunda ni sheria ya umoja wa kiraia. ili kuwalinda kisheria."
Ameongeza
kwamba "aliunga mkono wazo hilo", akiashiria nyakati alipokuwa Askofu
mkuu wa Buenos Aires, akisema japo alipinga ndoa ya wapenzi wa jinsia moja
katika sheria, aliunga mkono ulinzi wa kisheria kwa wapenzi wa jinsia moja.
Filamu ya Francesco, inayoangazi amaisha na kazi ya Papa Francis, ilioneshwa kama sehemu ya Tamasha la Filamu la Roma.
EmoticonEmoticon