Rais wa Marekani Donald Trump amesema siku zijazo zitakuwa "mtihani halisi" katika kupona kwake mambukizi ya virusi vya corona, katika ujumbe wa vidio alioweka katika ukurasa wa Twitter siku ya Jumamosi,(02.10.2020).
Video hiyo kutoka kwa rais Trump ,
ambaye anatibiwa katika hospitali ya jeshi, inakuja
baada ya taarifa zinazokinzana kusababisha mkanganyiko
kuhusiana na hali yake kiafya.
Trump alikuwa amevaa
suti bila tai na alikuwa amekaa wakati akirekodi ujumbe
wake huo. Alisikika kidogo akiwa anashindwa kuzungumza na
akipumua kwa taabu.
Nafikiri nitarejea hivi karibuni," alisema, na kuongeza kwamba anapambana kupona virusi hivyo kwa ajili yake binafsi na pia kwa dunia kwa ujumla.
— Donald J. Trump (@realDonaldTrump) October 3, 2020
"Ni
lazima nirejee kwasababu bado tunapaswa kuifanya
Marekani kuwa kubwa tena," alisema , akitumia kauli mbiu
ya kampeni yake.
Amesema
"anaanza kujisikia vizuri " lakini siku za
hivi karibuni zitakuwa mtihani halisi wa kupona kwake,
na amewashukuru waungaji mkono wake wa
ndani ya nje ya nchi hiyo kwa kumtakia
kupona haraka na "mapenzi yao makubwa."
Daktari wake Sean Conley aliwaambia waandishi habari mapema kuwa hali ya Trump inaendelea vizuri, na kusema timu ya madaktari "ina furaha kubwa kwa maendeleo anayopitia rais."
EmoticonEmoticon