Lil Wayne Ajikuta Katika Wakati Mgumu Baada Ya Kumsapoti Raisi Wa Marekani Trump

 

Legend wa Rap Duniani Lil Wayne, amejikuta katika wakati mgumu Kutoka Kwa wamarekani weusi Mitandaoni baada ya kupost picha akiwa na Rais Trump , kitendo kinachoonesha dhahili kuwa anamuunga mkono Rais huyo .

Lil Wayne alikutana na Rais Trump Siku ya Jana katika Ikulu ya Marekani , na kuzungumza nae kuhusu maboresho ya Sheria za Mahakama .

Kupitia picha hiyo , Lil Wayne aliandika ;- "Nimekutana na Rais Trump Siku ya Leo na kusungumza nae kuhusu hatua alizofikia katika kuboresha sheria za kimahakama . Amenisikiliza vyema na kuahidi kuwa ataenda kuboresha kila kitu "

Ujumbe huo wa Lil Wayne , umechukuliwa kama ni njia ya kumpigia Kampeni Trump katika uchaguzi Mkuu unaokuja , kitu kilichowakwaza Watu wengi hususani wamarekani weusi .


EmoticonEmoticon