Ubingwa huo
ni wa 17 katika historia ya LA Lakers na ubingwa wa nne wa NBA kwa nyota wa
timu hiyo LeBron James ambaye sasa ameshinda ubingwa akiwa na timu tatu
tofauti.
Timu ya Los Angeles Lakers imerudi katika kilele cha mpira wa
kikapu Marekani kwa kushinda ligi ya NBA msimu huu baada ya kuishinda Miami
Heat 106-93 katika mechi ya sita ya fainali za ligi hiyo. Lakers imeshinda
mechi 4-2.
Ni mara ya 17 kwa LA Lakers kuchukua ubingwa wa NBA ikiwa
sasa inafungana na timu ya Boston Celtics katika historia ya ligi hiyo.
Mara ya mwisho Lakers kufika fainali za NBA ilikuwa mwaka
2010, marehemu Kobe Bryant aliposhinda ubingwa wake wa tano. Bryant na binti
yake Gianna na watu wengine saba, walifariki katika ajali ya helikopta January
26.
Huu ni ubingwa wa nne kwa LeBron James, ambaye amecheza
katika fainali yake ya 10. James ameshinda ubingwa wa NBA na timu za Miami Heat
(2012 na 2013), na Cleveland Cavaliers (2016). James alimaliza mechi ya
Jumapili akiwa na pointi 28 na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa fainali za NBA
kwa mara ya nne.
Msimu huu wa NBA ulikuwa mrefu kuliko yote baada ya ligi kusimamishwa mwezi March kutokana na janga la corona. Baadaye mechi za NBA zilihamishiwa katika uwanja maalum katika mji wa Orlando, Florida ambako timu 22 zilizokuwa zikiongoza ligi zilialikwa kucheza mechi zao zote katika ukumbi wa Walt Disney World Resort.
EmoticonEmoticon