Maandamano Yazuka Kufuatia Mauaji Ya Mtu Mweusi Yaliotekelezwa Na Polisi (VIDEO)

 

Polisi mjini Philadelphia wamesema mamia ya wezi wamevamia na kuiba kwenye maduka ya biashara katika usiku wa pili wa ghasia zilizozuka baada ya polisi kumpiga risasi na kumuua mtu mweusi.

Polisi wa ziada pamoja na walinzi wa kitaifa wamepelekwa katika mji huo kutuliza ghasia. Maafisa wanasema polisi 30 wamejeruhiwa katika usiku wa kwanza wa ghasia hizo.

Polisi wanasema walimpiga risasi Walter Wallace, 27, alipopuuza amri ya kumtaka aangushe chini kisu alichokuwa ameshikilia mkononi.

Familia ya Bw. Wallace inasema alikuwa anakabiliwa na tatizo la afya ya kiakili.

Usiku wa Jumanne, polisi waliwaonya wenyeji kusalia ndani ya nyumba zao na kujiepusha na maeneo ya Riverfront Port Richmond kwasababu watu wamekuwa wakiiba katika maduka ya watu.

Ofisi ya Philadelphia ya kushughulikia hali ya dharura iliwashauri wakazi kusalia ndani kwasababu kulikuwa na "maandamano makubwa ambayo yamegeuka kuwa ya ghasia".

Kwa mujibu wa maafisa mjini Philadelphia, waandamanaji walijaribu kuweka vizuizi barabarani kwa kutumia vifaa vya kuzolea taka.

Polisi walilazimika kutumia maji ya kuwasha na fimbo kuwatawanya waandamanaji lakini walishambuliwa na waandamanaji hao.

Maduka katika mji huo yalifungwa mapema lakini yalivunjwa vio na mali kuibiwa usiku wa Jumanne.


EmoticonEmoticon