Maelfu
waandamana nchini Ufaransa kumuunga mkono Samuel Paty, mwalimu aliyekatwa
kichwa kwa kuonesha wanafunzi vibonzo vya Mtume Muhammad.
Watu
katika eneo la de la République mjini Paris walikuwa wameshika vipeperushi
vilivyoandikwa "Je suis enseignant" (Mimi ni mwalimu), wakati waziri
mkuu Castex amesema: "Sisi ni Ufaransa!"
Mwanaume
mmoja anayeitwa Abdoulakh A alipigwa risasi na polisi siku ya Ijumaa baada ya
kumuua bwana Paty karibu na maeneo ya shule karibu na mji wa Paris.
Watu 11 wamekamatwa kwa ajili ya uchunguzi. Hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu kukamatwa kwao. Ndugu wanne wakaribu wa washukiwa walishikiliwa kwa muda mfupi baada ya mauaji hayo.
Watu
wengine sita walishikiliwa siku ya Jumamosi , akiwemo baba wa wanafunzi ambaye
alitambulishwa na vyombo vya habari vya Ufaransa kuwa alikuwa muhubiri na
muislamu mwenye itikadi kali.
Rais
Emmanuel Macron alisema ukatwaji wa kichwa wa mwalimu katika kitongoji
kilichopo kaskazini magharibi mwa mji wa Paris -Ufaransa ni "Shambulio la
ugaidi wa uislamu" na mwalimu huyo aliuawa kwa sababu alikuwa anafundisha
uhuru wa kujieleza.
Mauaji hayo yanakuja baada ya shambulio la mwaka 2015 la Charlie Hebdo -ambalo lililengwa na washambuliaji kwa kuchapisha katuni za Mtume Mohammad.
EmoticonEmoticon