Idadi ya watu waliopoteza maisha
katika mafuriko na maporomoko ya ardhi katika maeneo ya kaskazini magharibi mwa
Italia imeongezeka hadi 6.
Kulingana na
ripoti ya Italia Rainews24, hali ya hewa ya mvua na upepo imeathiri vibaya
maisha ya kila siku katika mikoa ya Piedmont, Valle d'Aosta na Liguria
kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.
Miili ya
watu watatu imepatikana Liguria, mwili wa mtu mmoja umepatikana katika mto Roya
eneo la Piedmont, upande wa Ufaransa.
Imeripotiwa
kuwa watu 2 wamefariki jana katika maeneo ya Valle d'Aosta na Piedmont.
Kwa hivyo,
idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na janga hilo imefikia watu sita.
Imeelezwa
kuwa shughuli za utaftaji na uokoaji zinaendelea.
Barabara
nyingi na madaraja vimeharibiwa vibaya na mafuriko hayo Piedmont, Liguria na
Valle d'Aosta na kupelekea kusitishwa kwa usafiri katika maeneo mengi.
Onyo
limetolewa kuwa huenda kiwango cha maji katika mto Po kikaongezeka nchini humo.
Wakati huo huo, uongozi wa Piedmont na Ligurian umeitaka serikali kutangaza hali ya dharura katika maeneo hayo.
EmoticonEmoticon