Makubaliano Mapya Yatangazwa Nagorno-Karabakh

 

Armenia na Azerbaijan zimesisitiza dhamira yao ya kutafuta suluhisho la amani kwa mgogoro huo uliodumu miongo kadhaa na kukubali kujaribu kwa mara ya tatu kutekeleza mpango wa kuweka chini silaha. 

Makubaliano ya kusitisha mapigano yalioanza kutekelezwa leo saa mbili asubuhi yalitangazwa katika taarifa ya pamoja na serikali za Marekani, Armenia na Azerbaijan. 

Mikataba miwili ya awali ya kusitisha mapigano iliyosimamiwa na Urusi, ukiwemo mmoja wa mwishoni mwa wiki iliyopita, ilivunjika mara tu baada ya kuanza kutekelezwa, huku pande zote zikilaumiana kwa ukiukaji wake. 

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Marekani Mike Pompeo amesema jana usiku kuwa Marekani ilifanikisha mazungumzo makali na kuwa waziri wa mambo ya kigeni wa Armenia Zohrab Mnatsakanyan na mwenzake wa Azerbaijan Jeyhun Bayramov wamekubali kuanza kuutekeleza mpango huo leo. 

Na wakati Pompeo alikuwa akifanya mazungumzo tofauti na mawaziri hao, mapigano yalikuwa yamepamba moto Nagorno-Karabakh


EmoticonEmoticon