Mamia Ya Wanafunzi Wa Namibia Wakutwa Na Corona

 

Zaidi ya wanafunzi 300 nchini Namibia wameambukizwa virusi vya corona baada ya shule kufunguliwa.

Wizara ya Afya imesema wanafunzi walioambukizwa wengi wao wanasoma shule za mabweni.

Waziri wa Afya Kalumbi Shangula amesema muongozo uliowewa kuzuia kusambaa kwa maambukizi unastahili kuzingatiwa hasa katika maeneo ya shule.

Vyombo vya habari nchini humo vimeripoti mlipuko wa virusi vya corona katika moja shule iliyoko eneo la Oshikoto inayosadikiwa kuwa na idadi ya juu ya watu waliothibitishwa kuwa na virusi vya corona.

Namibia ilifunga shule mwezi Machi lakini zikafunguliwa tena mwezi Juni baada ya kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Covid-19.


EmoticonEmoticon