Marekani, India Zasaini Mkataba Wa Kushirikishana Taarifa Muhimu

 

India na Marekani zimesaini mkataba wa kijeshi unaohusu ushirikishanaji wa taarifa za siri huku kukiwa na mzozo wa mpaka kati ya serikali za Delhi na Beijing.

Kuweza kuzipata data hizo kunachukuliwa kama muhimu kwa ajili ya kuyaqpiga makombora , ndege zisizokuwa na rubani na kuyalenga maeneo.

Mkataba huo ulitangazwa baada ya mkutano wa mwaka wa "2+2" wa mazungumzo ya viongozi wa ngazi ya juu mjini Delhi Jumanne.

Wataalamu wanasema kuimarika kwa ushirikiano kati ya India na Marekani kunalenga kukabiliana na ushawishi wa China katika ukanda huo.

Waziri wa ulinzi wa Marekani Mark Esper alifanya mazungumzo na mwenzake wa India Rajnath Singh. Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo pia alikutana na waziri wa mambo ya nje wa India S Jaishankar.

"Katika kipindi cha miongo miwili, ushirikiano wetu umekua imara kwa vitendo, na kwa kwa kiwango cha umuhimu," Bw Jaishankar alisema Jumanne. Aliongeza kuwa mazungumzo yatawezesha nchi mbili kushirikiana kwa pamoja kwa mapana zaidi katika masuala ya usalama wa taifa ".

Makubaliano ya Mabadilishano ya kimsingi na Ushirikiano au BECA, ni miongoni mwa mikataba michache ambayo Marekani husaini na washirika wake wa karibu.

Yanairuhusu India kupata data au taarifa kwa kiwango cha zile za siri za anga za mbali na zile zinazohusiana na sayansi ya kutengeneza na kuendesha ndege, ambazo ni muhimu kwa hatua za kijeshi

Pande mbili pia zimesaini mikataba mingine kadhaa inayohusiana na nishati ya nuklia, sayansi ya dunia na tiba mbadala. Lakini BECA ndio mkataba muhimu zaidi miongoni mwake.

Unairuhusu Marekani "kutoa misaada ya vifaa vya majini na ya safari za anga katika ndege za Marekani zilizotolewa kwa India ", chanzo cha kijeshi cha India kililiambia Shirika la habari la Reuters - kwamba pia inamaanisha Marekani inaweza kuweka vifaa vyake vya manuwari za kijeshi katika ndege ilizozitoa kwa India.


EmoticonEmoticon