Mashambulizi Ya Urusi Yauwa Wapiganaji Wa Waasi Nchini Syria

 

Mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Urusi kwenye kambi ya mafunzo ya waasi wanaoungwa mkono na Uturuki nchini Syria limewauwa wapiganaji 78 na kujeruhi wengine zaidi ya 90. 

Kulingana na shirika linalofuatilia vita nchini Syria ndege za kivita za Urusi ziliielenga kambi hiyo ya Faylaq al-Sham iliyopo kaskazini magharibi ya jimbo la Idlib, ambayo ni ngome ya mwisho ya waasi nchini Syria. 

Shirika hilo lenye makao yake mjini London limesema viongozi wa kambi hiyo ni miongoni mwa watu waliouwawa na juhudi za uokozi zinaendelea. 

Mapema mwaka huu Uturuki na Urusi zilifikia makubaliano ya kusitisha mapigano kwenye jimbo la Idlib kwa lengo la kupunguza mashambulizi ya vikosi vya seirkali ya Syria ambayo yamesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makazi yao. 

Hata hivyo mkataba huo umeshindwa kutekelezwa kikamilifu na makabiliano bado yanaendelea.


EmoticonEmoticon