Mataifa ya Armenia na Azerbaijan yamekubaliana kusitisha mapigano katika eneo la Nagorno-Karabakh Katika taarifa yao wanadiplomasia wa juu kabisa wamesema hatua hiyo ina lengo la kubadilishana wafungwa na miili ya waliopoteza maisha huku ikiongeza kwa kueleza kwamba ufafanuzi zaidi utatolewa baadae.
Tangazo hilo linatolewa baada ya masaa 10 ya mazungumzo ya
kidiplomasia yaliofanyika nchini Urusi, ambayo yaliratibiwa na Waziri wa Mambo
ya Nje ya Urusi, Sergey Lavrov.
Lavrov amesema hatua hiyo ya kusitishia mapigano itafungua njia ya mazungumzo ya kuusuruhisha mgogoro huo.
Mapigano hayo ya sasa kati ya Azerbaijani na Armenian, ambayo yalianza Septemba 27 na kusababisha vifo vya mamia ya watu yanahusisha mzozo mkubwa kabisa wa wa miongo kadhaa kuhusu Nagorno-Karabakh.
Eneo hilo ambalo kiasili ni sehemu ya Azerbaijan lakini limekuwa katika udhibiti ya jamii ya wachache ya Warmenia, tangu kumalizika kwa mapigano ya kujitenga ya 1994.
EmoticonEmoticon