Mbwana Samatta Ashikilia Nafasi Ya 3 Baada Ya Messi Na Ronaldo Kumtangulia Orodha Ya Wachezaji Wanaofwatiliwa

 

Mtanzania Mbwana Samatta jina lake limeingia katika orodha ya Top 3 ya wachezaji waliofuatiliwa sana katika mtandao wa transfer market wakati wa usajili wa dirisha la majira ya joto.

Samatta anatajwa kuwa namba 3 baada ya Lionel Messi wa FC Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Juventus katika mtandao huo maarufu duniani. 

Hata hivyo jina la Samatta ambaye amedumu katika Ligi maarufu ya EPL kwa miezi sita, limeonekana kukuwa kwa haraka zaidi kutokana na uwezo na kuwa mchezaji pekee Tanzania aliyewahi kucheza EPL na sasa yupo Fenerbahce ya Uturuki kwa mkopo.


EmoticonEmoticon