Merkel Asikitishwa Ongzeka La Virusi Vya Corona Ulaya

 

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ana wasiwasi mkubwa kutokana na ongezeko la virusi vya corona katika eneo zima la Ulaya. 

Akizungumza katika mdahalo uliohusu urais wa Ujerumani wa Umoja wa Ulaya, amesema anaitazama kwa wasiwasi mkubwa hali ya kujirudirudia ya kuongezeka kwaidadi ya maambukizi karibu kila sehemu ya Ulaya. 

Kiongozi huyo wa Ujerumani amesema Ulaya haipaswi kuziweka kando hatua zilizopigwa kupitia sheria zilizowekwa miezi kadhaa za kudhibiti kuenea kwa maambukizi. 

Na ameongeza kusema kwamba sheria hizo hazikuwa rahisi kwa mtu yoyote lakini watu wengi wamepoteza maisha na kwasababu hiyo kuna umuhimu wa kuhakikisha kwamba hakutokei tena hali ya kufungwa kabisa kwa shughuli za kimaisha.


EmoticonEmoticon