Mwanamke Wa Kwanza Kupewa Hukumu Ya Kifo Marekani Toka Miaka 70

 

Marekani inatekeleza hukumu ya kifo kwa mfungwa wa kike kwa mara ya kwanza katika kipindi cha karibu miaka 70, kulingana na Wizara ya Sheria.

Lisa Montgomery alimyonga mwanamke mjamzito huko Missouri kabla ya kumkata mama huyo tumbo lake na kumtoa mtoto aliyekuwa amembeba mwaka 2004. Anatarajiwa kuchomwa au kudungwa sindano ya sumu Desemba 8.

Mwanamke wa mwisho kuhukumiwa kifo na serikali ya Marekani alikuwa Bonnie Heady, aliyekufariki dunia kwenye chumba cha gesi huko Missouri mwaka 1953, kulingana na kituo cha taarifa za adhabu ya kifo.

Hukumu ya serikali dhidi ya Brandon Bernard, ambaye pamoja na washirika wake waliwauwa mawaziri wawili vijana mwaka 1999, pia imepangiwa kutolewa Desemba.

Mwanasheria mkuu William Barr alisema uhalifu huo "ni vitendo vya kinyama". Mwaka jana, utawala wa Trump ulisema kuwa utaanza tena kutekeleza hukumu ya kifo.


EmoticonEmoticon