Shirika la
Marekani la anga za juu (Nasa) limetangaza rasmi mpango wake wa kurejea tena
mwezini utakaogharimu dola bilioni 28b ifikapo mwaka 2024.
Kama
sehemu ya mpango unaojulikana kama Artemis, Nasa itawapeleka mwanaume na
mwanamke mwezini kwa mara ya kwanza tangu binadamu kufika huko mwaka 1972.
Lakini
mpango huo utategemea na iwapo bunge la Marekani litaidhinisha jumla ya dola
bilioni 3.2 za kununua vifaa vitakavyotumiwa katika safari hiyo.
Wanaanga
watasafiri kwenye chombo kilicho na muundo wa maalum kinachofahamika kama Orion
na ambacho kitarushwa angani kupitia roketi itakayotumia mfumo unayojulikana
kama SLS.
Akizungumza
mnamo mwezi Septemba tarehe 21, msimamizi wa Nasa Jim Bridenstine alisema:
"Dola bilioni 28 zitatumiwa kugharamia shughuli zitakazohusiana na safari
hiyo katika kipindi cha miaka minne kufadhili mpango wa Artemis kwenda mwezini.
Ufadhili
wa SLS, ufadhili wa Orion, binadamu watakaotumia chombo hicho kwenda mwezini -
vyote hivyo ni vitu vitakavyokuwa vimejumuishwa kwenye mpango wa Artemis
."
Lakini alifafanua kuwa: "Bajeti iliyowasilishwa mbele ya mikutano yote miwili ya bunge kwa sasa inajumuisha dola bilioni 3.2 ya mwaka 2021 itagharamia mfumo utakawapeleka binadamu mwezini. Ni muhimu sana tupate fedha hizo, dola bilioni hizo 3.2."
EmoticonEmoticon