Ndege Za Kijeshi Zagongana Na Kusababisha Vifo Vya Watu 9 Afghanistan

 

Ajali ya ndege mbili za kijeshi aina ya helkopta za Afghanistan zimesababisha wanajeshi kujeruhiwa huko kusini mwa jimbo la Helmand na wengine tisa kufariki.

Wote waliofariki walikuwa ndani ya ndege hizo, maofisa wamesema.

Tukio hilo limetokea mapema Jumatano katika kitongoji cha Nawa na ajali hiyo ilisababishwa na tatizo la kiufundi.

Eneo hilo limekuwa na mapigano hivi karibuni kati ya Taliban na jeshi la serikali ya Afghanistan , wakiungwa mkono na wanajeshi wa angani kutoka Marekani.

Mapigano hayo yamekuwa yakiendelea pembezoni mwa mji wa Lashkar Gah ambako kulikuwa tayari kumedhibitiwa

Umoja wa mataifa unasema zaidi ya watu 35,000 wamelazimika kuhama makazi yao huko Helmand.


EmoticonEmoticon