Nokia Kufungua Internet Mwezini

 

Miaka michache ijayo watafiti watakaofika kwenye mwezi hawatashindwa kupatikana katika simu kwa sababu internet itakwepo!

Nokia imeshinda dili la dollar Million 14.1 sawa na Billion 32.7 kufunga mawasiliano katika mwezi. 

Project hii ambayo kampuni iliyokuwa maarufu hasa katika kuuza simu, kampuni ya Nokia imepata nafasi hii na itashirikiana na NASA kutengeneza mawasiliano katika Mwezi.

Nokia imeshinda project hii na itaanza kufunga 4G/LTE katika mwezi katika mradi wa “Tipping Point” kuboresha speed ya utafiti kwa kuboresha mawasiliano katika anga. 

Internet hii itasaidia mawasiliano ambayo yatatumika na satelittes, magari ya utafiti (lunar rovers), watafiti na mitambo ambayo itakuwa ni rahisi kuunganishwa mawasiliano na kusaidia kuongeza ufanisi wa utafiti wa anga.

Changamoto ya vifaa vya mawasiliano hayo itabidi kutumia materials ambayo yanahimili mionzi, minara imara inayoweza kuduma kwa muda mrefu katika mwezi, na materials ambayo hayataharibika kwa joto kali. 

Ni good news kwa Nokia kwa sababu kampuni hii ilikuwa imeshuka ufanisi hasa kwa kupunguza umaarufu wake katika kuuza simu.


EmoticonEmoticon