Offset Na Cardi B Warudiana, Cardi B Aeleza Sababu Za Kumsamehe

 

Ikiwa ni mwezi Mmoja tu tangu aombe talaka , Rapa Cardi B na Mume wake Offset wameonesha kurudisha Mapenzi yao upya , baada ya kusheherekea Birthday ya Card B huko Las Vegas Wiki iliyopita .

Kupitia Ukurasa wake wa Instagram , Rapa Card B aliamua kuingia LIVE na kuwaelezea mashabiki zake ni sababu zipi zimemfanya aamue kurudiana na Offset ambae amezaa nae mtoto Mmoja .

" Nilianza kummiss sana .. ni ngumu sana kukaa bila kuongea na rafiki yako /Mtu wako umpendae na Pia siwezi kuishi bila kufanya mapenzi " - ameeleza Cardi B

Card B Pia ameeleza asingeweza kukataa zawadi ya Gari aina ya Rolls Royce ambayo Mume wake huyo alimzawadia Siku ya Birthday, Licha ya wawili hao kutokua na maelewano Kipindi hicho .

"Mlitaka nifanyeje ? Jamaa kaninunulia Rolls Royce kwenye Birthday yangu, mlitaka nilikatae ? " - alihoji Cardi B .


EmoticonEmoticon