Pande Mbili Hasimu Zatia Saini Mkataba Wa Amani Libya

 

Pande hizo mbili zinazohusika na mgogoro wa nchini Libya zimekubaliana kutia saini mkataba wa kudumu wa kusimamisha mapigano baada ya kufanyika mazungumzo ya siku tano yaliyosimamiwa na Umoja wa Mataifa. 

Umoja wa Mataifa umeyaita makubaliano hayo kuwa ya kihistoria baada ya mapigano ya miaka kadhaa yaliyoigawanya Libya katika pande mbili. 

Pamoja na hatua nyingine, makubaliano hayo yanaagiza kuondolewa kwa mamluki wa kutoka nje na kuwezesha kufanyika mazungumzo mwezi ujao ili kutafuta suluhisho la kudumu.

Libya ilitumbukia katika vurumai baada ya nchi za NATO kuivamia nchi hiyo mnamo mwaka 2011 na kumwondoa kiongozi wake kanali Muammar Gaddaffi aliyetawala kwa muda mrefu. 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema makubaliano yaliyofikiwa ni muhimu sana, hata hivyo ameeleza kuwa juhudi zaidi zinahitajika.


EmoticonEmoticon