Polisi wa
zamani wa Marekani aliyeshitakiwa kwa mauaji ya mwanamume mweusi ambaye hakuwa
amejihami George Floyd ameachiliwa kutoka jela kwa dhamana.
Derek
Chauvin alitoa Bondi ya dola milioni moja sawa na (Euro 774,000) na kuachiliwa
Jumatano asubuhi, nyaraka za mahakama zinaonesha.
Afisa
huyo mzungu alirekodiwa kwenye kanda ya video akipiga goti kwenye Shingo ya Bw.
Floyd kwa karibu dakika nane kabla afariki dunia Mei 25.
Kifo cha
Bw. Floyd kilisababisha maandamano makubwa nchini Marekani kushinikiza mageuzi
katika idara ya polisi, yakiongozwa vugu vugu la Black Lives Matter.
Bw. Chauvin
alitolewa kizuizini muda mfupi kabla ya saa tano na nusu asubihi (saa za
Marekani) siku ya Jumatano, kwa mujibu wa ofisi ya polisi ya kaunti ya
Hennepin.
Ben
Crump, wakili na mwanaharakati wa kutetea haki anayewakilisha familia ya Bw.
Floyd, alisema kuachiliwa kwa Chauvin kwa dhamana "kunatukumbusha kwa
machungu" kwamba "bado tuko mbali kupata haki kwa George".
"Japo
George Floyd alinyimwa haki akiwa hai, hatututarudi nyuma hadi atendewe haki
akiwa amekufa," Bw Crump alisema.
Kwa
sasa, maafisa wote wanne wamepangiwa kuhukumiwa pamoja mwezi Machi, lakini jaji
anatafakari uwezekano wa kila mmoja wao kuhukumiwa kivyake.
Tukio
lililosababisha kushitakiwa kwao lilitonesha makovu ya ubaguzi na ukosefu wa
usawa nchini Marekani.
Maandamano ya Black Lives Matter - ambayo baadhi yallikumbwa na vurugu - ilikuwa suala la kisiasa kuelekea uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba Marekani.
EmoticonEmoticon