Raisi Wa Marekani Trump Akataa Kushiriki Mdahalo Mtandaoni

 

Muda mchache baada ya Tume kutangaza kuwa mdahalo wa pili wa Wagombea Urais utafanyika kupitia mtandao, Rais Trump amesema hatoshiriki kwasababu uamuzi huo unalenga kumlinda mpinzani wake, Joe Biden.

Tume imesema imeamua kubadili mfumo wa mdahalo huo wa Oktoba 15 ili kulinda afya za washiriki baada ya Rais Trump kupata maambukizi ya COVID19 hivi karibuni.

Kwa upande wao, timu ya kampeni ya Biden imekubali uamuzi huo na kusema Mgombea huyo atashiriki katika mdahalo ili kuongea moja kwa moja na Wamarekani.


EmoticonEmoticon