Raisi Wa Marekani Trump Na Mke Wake Wapata Corona

Raisi wa Marekani Donald Trump na mke wake wamepatikana na virusi vya corona baada ya kuwa kwenye karantini.

Rais Donald Trump wa Marekani amesema kwamba yeye na mke wake Melania Trump wamepatikana na virusi vya corona na wako kwenye karantini.

Ametoa tangazo hilo kwenye mtandao wa Twitter.

Tangazo hilo linawadia baada ya Bwana Trump na wasaidizi wake wawili kuthibitishwa kuambukizwa virusi vya corona.

Hope Hicks, 31, mshauri wa rais amekuwa msaidizi wa karibu wa Bwana Trump kupatikana na virusi vya corona hadi hivi sasa.

Bi. Hicks alisafiri na yeye kwa ndege ya kijeshi kwenda kwenye mdahalo wa Televisheni uliofanyika Ohio mapema wiki hii. 


EmoticonEmoticon