Rais wa
Nigeria Liberia George Weah ameiomba Marekani kusaidia katia uchunguzi wa
mauaji ya ajabu ya maafisa wa ngazi ya juu katika nyadhifa zinazohusiana na
masuala ya fedha nchini mwake, lineripoti shirika la habari lenye uhusiano na
serikali yaLiberia.
Vifo vya
maafisa hao vimeibua tetesi za kampeni ya mauaji, kulingana na taarifa ya
shirika la habari la AFP.
LINA
lilimnukuu Bwana Weah akiwataka watu kuacha kubashiri, na kusubiri matokeo ya
uchunguzi.
Bwana Weah
alikuwa amemuagiza Waziri wa fedhaFrank Musa Dean kuratibu juhui zake na
washirika wa serikali , ikiwa ni pamoja na LINA limeripoti.
Ilimtaja
mmoja wa maafisa aliyeuawa kuwa alikuwa mkuu wa Shirika la ukaguzi wa ndani ,
Emmanuel Nyeswua.
Wengine
walikuwa wafanyakazi wa Mamlaka ya mapato nchini Liberia, lakini LINA
halikuwataja.
Shirika la
AFP limeripoti kuwa ni watu wanne – na sio watatu waliokufa katika kipindi cha
wiki moja tu.
Walikuwa ni:
Bwana
Nyeswa, ambaye alipatikana akiwa amekufa katika katika makazi yake yaliyopo
katika mji mkuu , Monrovia, Jumamosi.
Afisa katika
mamlaka ya mapato ya Liberia aliyeuawa katika ajali ya gari katika mji mkuu
Monrovia tarehe 4 Octoba
Maafisa wengine wawili zaidi katika mamlaka ya ukusanyaji wa kodi ambao walipatikana wakiwa wamekufa ndani ya garisiku iliyofuatia.
Credit:Bbc
EmoticonEmoticon