Rais wa Nigeria ametoa wito kwa raia wa nchi hiyo kuacha maandamano na kushirikiana na serikali katika kusuluhisha matatizo yanayoikumba nchi hiyo, akisisitiza kwamba serikali imesikia matakwa ya waandamanaji na inayashughulikia.
Buhari amehutubia nchi wakati maafisa wa usalama katika mji
mkuu wa Lagos wanapata wakati mgumu kutekeleza amri ya watu kusalia nyumbani
kwao katika juhudi za kumaliza maandamano ya kupinga polisi kutumia nguvu
kuzidi kiasi.
Katika
hotuba yake kwa taifa Alhamisi jioni saa za Nigeria, Buhari aliwaomba vijana
“kuacha maandamano na kukubali kushirikiana na serikali kutafuta suluhisho.”
Buhari ameomba jumuiya ya
kimataifa “kujua ukweli kwa ukamilifu kabla ya kukimbilia kufanya maamuzi.”
Maandamano ya kupinga
polisi kutumia nguvu ambayo yameingia wiki ya pili yalikuwa ya amani hadi pale
polisi walipowapiga risasi waandamanaji.
Polisi wanasema baadhi ya wahalifu walikuwa wameanza kutumia fursa ya maandamano kufanya uhalifu.
EmoticonEmoticon