Rashford Wa Man United Apata Tuzo Ya Heshima

 

Mshambuliaji wa Manchester United na England, Marcus Rashford amepata tuzo ya heshima ya (MBE) inayotolewa na Malkia wa Uingereza kwa mchango wake alioutoa kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini Uingereza wakati wa janga la COVID-19.

Kampeni ya Mchezaji huyo, mwenye miaka 22, akishirikiana na serikali iliwezesha watoto karibu milioni 1.3 nchini Uingereza kupata chakula cha bure katika shule mbalimbali wakati wa janga la virusi vya Corona hasa kweney msimu wa joto.


EmoticonEmoticon