Eminem ameendelea kuandika historia
mpya kila uchwao, ngoma yake "Lose Yourself" imefikisha jumla ya
Streams Bilioni 1 kwenye mtandao wa Spotify hivyo kuifanya kuwa ngoma ya kwanza
ya Hip Hop iliyotoka miaka ya 2000 kufikia mafanikio hayo.
Wimbo huo ulitoka
Oktoba 28 mwaka 2002 chini ya label ya Aftermath, Shady na Interscope. Ukiacha
mengi makubwa yaliyofanywa na Lose Yourself kama kuwa wimbo wa kwanza wa Hip
Hop kupata tuzo ya Oscar 'Best Original Song' pia kuna hizi Facts 3 za kufahamu
kuhusu wimbo huu.
1. Eminem aliandika
mashairi ya wimbo huu wakati akitengeneza filamu ya maisha yake iitwayo 8 Mile
mwaka 2002.
2. Karatasi
iliyotumika kuandika mashairi ya wimbo huo ilitokea pia kwenye filamu ya 8
Mile. Hata hivyo karatasi hiyo baadaye ilipigwa mnada kwenye mtandao wa eBay,
iliuzwa $10,000 sawa na takribani milioni 23 za Kitanzania.
3. Mwaka 2015 Jaji
alinukuu (quote) mashairi ya wimbo huo kwenye Kesi akiwa mahakamani. Kwenye
Mahakama Kuu ya mjini Washington D.C, Jaji Yvonne Williams aliwahukumu mapacha
wawili waliomshambulia mwanaume mmoja mjini Brooklyn.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon