Rihanna
aomba msamaha kwa kutumia Hadith ya Kiislamu kwenye onesho la nguo za ndani za
kampuni yake ya Fenty.
Alianza kukosolewa vibaya mtandaoni
kwa kutumia wimbo uaojulikana kama Doom wa msanii Coucou Chloe, ambao
unajumuisha maudhui ya Kiislamu yanayofahamika kama Hadith.
Rihanna amesema utumiaji wa nyimbo
hiyo ulikuwa "ukosefu wa umakini."
Hadith ni sehemu ya baadhi ya maneno
ambayo yanaaminika kuzungumzwa na mtume Muhammad.
Baada ya kitabu takatifu cha Quran,
Hadithi inachukuliwa kuwa baadhi ya meneno muhimu kwenye dini ya Kiislamu.
Mashairi ya Kiarabu ya wimbo huo ni
sehemu ya Hadith kuhusu siku ya kiyama.
Baadhi ya wafuasi wake wa Kiislamu
walianza kuhoji matumizi ya wimbo huo kwenye onesho lake lilioneshwa moja kwa
moja kupitia mtandao wa Amazon Oktoba 2.
Aidha, Coucou Chloe pia ameomba
msamaha na kusema hakujua kwamba wimbo huo una mashairi ya dini ya Kiislamu.
Lakinihii sio mara ya kwanza Rihanna
kushutumiwa kwa kufanya mambo yasiokubalika yanayolenga dini ya Kiislamu.
Mwaka 2013, aliombwa kuondoka katika msikiti mmoja huko Adu Dhabi baada ya kuonekana akipiga picha zisizofaa".
EmoticonEmoticon