Saad al-Hariri Ateuliwa Tena Kuwa Waziri Mkuu Wa Lebanon

 

Rais wa Lebanon Michel Aoun amemteua mwanasiasa Saad al-Hariri kama waziri mkuu na kumtaka aunde serikali mpya kukabiliana na mzozo mbaya zaidi tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe vya nchi hiyo kati ya 1975 na 1990. 

Hariri amepata uungwaji mkono wa wabunge walio wengi katika mashauriano na Aoun. 

Anakabiliwa na changamoto kubwa kushawishi siasa za kugawana madaraka za Lebanon, na kukubaliana juu ya baraza, ambalo linapaswa kushughulikia orodha inaoyoongezeka ya masaibu, yakiwemo mgogoro wa mabenki, mporomoko wa sarafu ya nchi, umaskini unaoongezeka na mzigo wa madeni ya taifa.


EmoticonEmoticon