Serikali ya
Sudan na makundi ya waasi leo yametia saini mkataba wa kihsitoria wa amani
unaolenga kumaliza miongo kadhaa ya vita vilivyohujumu maisha ya mamia kwa
maelfu ya watu.
Kulikuwa na shamra shamra
wakati wawakilishi wa serikali na makundi ya waasi walipotia saini hati ya
mkataba huo ikiwa ni takriban mwaka mmoja tangu kuanza kwa mazungumzo ya kusaka
amani baina ya pande hizo.
Hafla ya kutia saini
imefanyika kwenye mji mkuu wa taifa jirani la Sudan Kusini, Juba, na
kuhudhuriwa na wawakilishi wa Chad, Qatar, Mirsi, Umoja wa Afrika, Umoja wa
Ulaya na Umoja wa Mataifa.
Mkataba huo unajumuisha
masuala kadhaa ikiwemo umiliki ardhi, mgawanyo wa madaraka na mapato ya
serikali na kurejea kwa wakimbizi na raia waliopoteza makaazi wakati wote wa
mzozo.
Aidha, chini ya hati ya makubaliano, wapiganaji wa makundi ya waasi kutoka majimbo ya Darfur, Kordofan ya Kusini na Blue Nile watajumuishwa taratibu kwenye vikosi vya jeshi la serikali.
EmoticonEmoticon