Shirika La Afya Duniani WHO Lasema Athari Ya Corona Kwa Afya Ya Kiakili Ni Kubwa

 

Shirika la afya duniani limeonya kuwa janga la virusi vya corona lina athari kubwa katika huduma za afya ya akili kote ulimwenguni kabla ya mchakato mkubwa wa kuchanga pesa. 

Shirika hilo limeonya kuwa afya ya akili imepuuzwa wakati wa janga hilo na kutaja utafiti uliofanywa kati ya mwezi Juni na Agosti uliofichuwa kutatizwa pakubwa kwa huduma hizo katika mataifa 93. 

Shirika hilo la WHO limeendelea kusema kuwa huku asilimia 83 ya mataifa 130 yaliyofanyiwa utafiti yakiwa yamejumuisha afya ya akili katika mpango wa kushughulikia janga la virusi vya corona, ni asilimia 17 pekee iliyokuwa imeweka pesa zote zinazohitajika. 

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari kwa njia ya mtandao, mkurugenzi wa afya ya akili katika shirika hilo Devora Kestel, amesema kuwa hilo ni suala lililosahaulika la ugonjwa wa COVID-19 na kusisitiza haja ya kuongezwa kwa ufadhili mara moja.


EmoticonEmoticon