Tazama Samaki Aina Ya Albino Aliyevuliwa Na Mvuvi

 

Mvuvi mmoja nchini Uingereza amesema amepata bahati ya kuvua samaki aina ya papa mwenye albinism (zeruzeru)  akapiga naye picha kisha kumrudisha tena baharini.

Kwa mujibu wa shirika la habari la TMZ, Jason Gillespie, amesema alikuwa anavua samaki na marafiki zake karibu na maeneo ya ‘Isle of Wight’ ndipo alipomvua papa huyo mwenye albinism ya rangi nyeupe tupu ambaye alikuwa na urefu wa futi 3.

“Nimekuwa nafanya kazi ya uvuvi kwa kipindi cha miaka 30, kamwe sikuwahi kuona samaki kama huyu, nilimuachia kwa sababu ni spishi inayolindwa, nilijua ilikuwa kitu maalum kwa hiyo nikapiga naye picha kisha nikamuachia baharini.  Ilikuwa ni nafasi kwangu sijui niseme nini, ni samaki wa maisha, mmoja kati ya milioni, ” amesema Jason Gillspie. 

Inaaminika Jason Gillespie ndiye mvuvi pekee aliyepata udhibitisho wa papa mwenye albinism japo mwenyewe amesema aliwahi kusikia mvuvi mwingine kutoka Wales ambaye alivua papa kama huyo mwaka mmoja uliopita ila alikuwa mdogo.

Papa hao wenye albinism huishi tofauti na papa wengine kutokana na rangi zao, pia huwa hawaonekani kwa sababu wanajificha sana wakati wa uvuvi.


EmoticonEmoticon