Tory Lanez amefunguka kwa mara ya
kwanza tangu asomewe mashtaka yake ya kumshambulia rapa Megan Thee Stallion,
mashtaka ambayo huwenda yakamuweka gerezani hadi miaka 22.
Kupitia ukurasa
wake wa twitter, Tory Lanez alizungumzia mashtaka hayo na kuweka wazi kwamba
muda utazungumza na ukweli utajidhihirisha.
"Muda utasema,
na ukweli utadhihirika. Nina imani yote kwa Mungu kuonesha yote haya. Upendo
kwa mashabiki wote na watu ambao wameendelea kubaki na mimi na kuufahamu moyo
wangu. Mashtaka sio kukutwa na hatia. Kama uliniunga mkono mimi au Megan katika
hili, ninalithamini sana hilo." ilisomeka tweet ya Tory Lanez.
Tory Lanez atafikishwa mahakamani Oktoba 13 mwaka huu na kama akikutwa na hatia ya mashtaka yote yakiwemo ya kumiliki silaha kinyume cha sheria pia kukutwa na silaha yenye risasi kwenye gari, basi atahukumiwa kifungo cha miaka 22 gerezani.
EmoticonEmoticon