Travis Scott Athibitisha Kulamba Dili La PS5

 

Rapa Travis Scott alikuwa mtu wa kwanza kutuonesha mikono yake imeikamata PS5, wengi walijiuliza ni kwanini lakini hatimaye majibu yamepatikana.

Travis Scott ametangaza ushirika wake kibiashara na PlayStation katika bidhaa zijazo za PS5 ambapo amesema amekuwa sehemu ya timu kubwa ya ubunifu (creative partner) wa bidhaa hizo.

Kwenye maelezo yake wakati akithibitisha ushirika huo, Travis Scott amesema

"Ninashkuru sana na nina furaha kubwa kuweza kuleta mkakati wangu wa kiubunifu na maono kwenye maendeleo ya bidhaa kubwa kama hii. Siku zote nimekuwa shabiki mkubwa wa PlayStation na chapa yao waliyoitengeneza. Huu ni mwanzo tu wa ushirikiano wetu mzuri." alisema Travis Scott kwenye taarifa kwa waandishi wa habari.


EmoticonEmoticon