Trey Songz Apata Maambukizi Ya Corona Covid-19

 

Star wa R&B Duniani Trey Songz ametangaza kukutwa na Maambukizi ya Covid-19 , na kuahidi kuwa atajitahidi kujitenga na wale wote anaowapenda ili kuweza kuwalinda na Maambukizi wa Virusi ivyo .

Akizungumza kupitia video ambayo ameshare kupitia Ukurasa wake wa Instagram, Trey amesema kuwa anahisi aliweza kupata maambukizi hayo Kutokana na kushiriki maandamano Mbalimbali ambayo yamefanyika hivi karibuni nchini Marekani.

“Nina mtoto Mdogo , ivyo ilinibidi niwe napima mara kwa mara . Mara hii ya Mwisho kupima nikekutwa na Maambukizi. Hivyo Ntajitahidi kujifungia , kujitenga na kukaa Karantini mpaka Pale ntakapopona “ - Amesema Trey Songs .


EmoticonEmoticon