Trump Arejea Kwenye Kampeni Baada Ya Kupona Corona

 

Rais Donald Trump wa Marekani amerejea tena kwenye kampeni za uchaguzi mkuu kwa kufanya mkutano wa kwanza jimboni Florida siku kadhaa tangu alipogundulika na maambukizi ya virusi vya corona. Rais Trump aliwasili kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika eneo la wazi huko Sanford; Florida bila ya kuvaa barakoa.

Mkutano wa kampeni mjini Florida,  jimbo ambalo ni muhimu kwa Trump kushinda, unafungua njia ya mikutano zaidi iliyopangwa kufanyika wiki hii kwenye majimbo ya Pennsylvania, Iowa na North Carolina. 

Akiwahutubia maelfu ya wafuasi wake waliosimama bega kwa bega wengi wakiwa bila barakoa, Trump amesema afya yake imeimarika na yuko huru kukutana tena na wapiga kura bila ya kuwa na wasiwasi wowote.

 "Nimetiwa nguvu kwa maombi yenu na nimefarijika kwa uungaji wenu mkono. Tunaungwa mkono vya kutosha. 

Na tuko hapa lakini tunaenda kukamilisha, tutalifanya taifa hili kuwa kubwa kuliko ilivyokuwa hapo kabla." alisema rais Trump.


EmoticonEmoticon