Rais wa Marekani Donald Trump amepelekwa Kituo cha Matibabu cha Jeshi la Kitaifa cha Walter Reed baada ya kuambukizwa ugonjwa wa COVID-19.
Ameahirisha mikutano yote ya kampeni kabla ya
uchaguzi. Rais wa
Marekani Donald Trump Ijumaa amepelekwa katika hospitali ya kijeshi kupatiwa
matibabu baada ya kukutikana na ugonjwa wa COVID-19.
Trump amehamishiwa katika
hospitali ya Walter Reed saa 17 baada ya kugunduliwa kuwa na ugonjwa huo.
"Hali yangu
inaendelea vizuri," Trump ameonekana akisema katika vidio fupi aliyoituma
kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Kellyanne Conway, meneja
wa kampeni za Trump za 2016, amesema naye pia amepata ugonjwa wa COVID-19.
"Dalili zangu ni za mbali (kikohozi kidogo) na ninajisikia vizuri.
Nimeanza mchakato wa kujitenga kwa kushauriana na madaktari," Conway
ameandika Twitter.
Msemaji wa Ikulu ya White
House Kayleigh McEnany amesema Trump atafanya kazi katika chumba maalum
hospitalini kwa siku chache zijazo kama hatua ya tahadhari.
Trump kupewa dawa bado
inayofanyiwa majaribio
Inasemekana kwamba Trump
mwenye umri wa miaka 74, anasumbuliwa na homa na kwamba atapewa dawa ambayo
bado inafanyiwa majaribio.
Trump, ambaye amekuwa
akikana kishio cha virusi vya corona tangu janga hilo lilipoanza, aliandika
kwenye Twitter mapema Ijumaa kwamba yeye na mkewe Melania watalazimika
kujitenga baada ya kupimwa na kukutwa na virusi hivyo, ambavyo vimeua zaidi ya
Wamarekani 200,000 na kuharibu vibaya uchumi wa taifa hilo.
Trump yuko
katika hatari kubwa kwa sababu ya umri na uzito wake wa mwili.
Ugonjwa wa COVID-19
umesimamisha kampeni za rais huyo ikiwa zimebakia siku 31 pekee hadi siku ya
uchaguzi. Wasimamizi wa kampeni za Trump wamesema mikutano yote na hafla
nyingine zilizokuwa zimepangwa zitaahirishwa au zitafanyika mtandaoni.
Rais huyo wa Marekani wa chama cha Republican amepata ugonjwa wa COVID-19 akiwa katikati ya kampeni kuelekea uchaguzi wa mwezi Novemba ambapo atachuana na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden.
EmoticonEmoticon