Trump Na Biden Washambuliana Katika Kampeni

Rais Donald Trump na mpinzani wake wa chama cha Democratic Joe Biden walionyesha misimamo tofauti ya kukabiliana na janga la virusi vya corona walipokuwa wakiwahutubia wafuasi wao Alhamis katika jimbo muhimu la Florida. 

Huku uchaguzi nchini humo utakaofanyika Jumanne ukikaribia maelfu ya watu wengi wao wakiwa bila barakoa walikusanyika katika mkutano wa Rais Trump ambapo kiongozi huyo alimkejeli mpinzani wake.

"Hebu fikiria, nipoteze uchaguzi kwa mtu huyu? inawezekana kweli?" alisema Trump.

Rais huyo wa Marekani ameendelea kupuuza janga la Covid 19 akiwaambia wafuasi wake kwamba hata watakapoambukizwa, watapona tu kama alivyopona yeye baada ya kuambukizwa.

Trump amefanya tukio kubwa la kusambaza virusi vya corona

Masaa machache baadae Biden aliwasili katika eneo hilo kuwahutubiawafuasi wake waliokuwa ndani au karibu ya magari yao wakiwa wamevaa barakoa kwa ajili ya kupunguza kusambaa kwa virusi hivyo, ingawa hakukuwa na umbali wa mtu hadi mtu kila wakati.

Biden amemkosoa Trump kwa kufanya kile alichokiita ni "tukio kubwa la kusambaza virusi vya corona" na akashambulia matamshi ya kila mara ya rais huyo kwamba Marekani imevuka kipindi kibaya cha janga la virusi vya corona, licha ya ongezeko la maambukizi kote duniani.

"Donald Trump ameipeperusha bendera nyeupe, ameziacha familia zetu na kushindwa kukabiliana na virusi vya corona," alisema Biden. "Ila Wamarekani hawafi moyo, hatutofi moyo," aliongeza mgombea huyo wa Republican.

Janga la Covid-19 limesababisha maafa mengi Marekani ambapo kufikia sasa zaidi ya watu 227,000 wamefariki dunia. Fauka ya hayo mamilioni ya watu wamepoteza kazi.

Jopokazi la White House linaonya kuhusiana na mwendeleo wa maambukizi ya virusi vya corona kwa kiwango kikubwa, ikiwemo katika majimbo ambayo yatakuwa ni muhimu mno katika uchaguzi. 


EmoticonEmoticon