Rais wa Marekani Donald Trump amesema
kuwa ikitokea akashindwa katika Kura za Uchaguzi wa Urais Mwaka huu dhidi ya
Joe Biden , atafikiria kuihama nchi hiyo.
Trump ameyasema
hayo katika Moja ya mkutano wake wa Kampeni za Urais , na kusisitiza kuwa
itakuwa ni fedheha sana kwake kushindwa dhidi ya Mwanasiasa mbovu katika
hitoria ya nchi hiyo (akimaanisha Joe Biden).
"Mnajua kuwa
Nina Presha sana kwasababu nagombea dhidi ya Mwanasiasi mbovu katika historia
ya nchi hii , hivyo nikishindwa itakuwa ni aibu sana katika maisha yangu .
Ikiwezekana naweza nikahama kabisa na nchi " - amesema Rais Trump
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon