Mahakama Yamtaka Tory Lanez Kukaa Mbali Na Megan Thee Stallion

Rapa Tory Lanez ameamuliwa na Mahakama kukaa mbali kabisa na Meg Thee Stallion , katika kipindi hiki ambacho Kesi yake ya Kumshambulia Mrembo huyo kwa bunduki inaendelea .

Amri hiyo imetolewa Katika Mahakama huko Los Angeles, baada ya kesi inayomkabili Tory kusikilizwa kwa mara ya Kwanza Siku ya Jana Jumanne .

Tory Lanez anakabiliwa na Mashitaka ya Kumshambulia Meg Thee Stallion kwa risasi , Mwishoni mwa Mwezi Septemba , na amekamatwa Rasmi kuhusu kesi hiyo Mwishoni mwa Wiki iliyopita .

Tory anatarajiwa kutoa dhamana ya Tsh Milion 440 , ili aweze kuisubiria tarehe ya kesi yake akiwa nje ya Gereza.


EmoticonEmoticon